..
..
| Hasira
ni hisia hatari sana katika kazi yako –– tunaisindaje. Kama
binadamu tuna hisia, na hasira ni moja ya hsia hizo. Ni sahihi kuwa na
hasira; Tusijisikie vibaya au aibu kuwa na hasira. Hasira yenyewe ni hisia
ya kawaida kwa binadamu. tunatakiwa tuikubali pale inapotutokea. |
....... |
Tunafanyeje
tunapopata hasira? hii itatuathiri tunapoiwezesha jamii, kuratibu wanaojitolea
au kuwaongoza wafanyakazi. Endapo mteja, mtu anaejitolea, mfanyakazi au
mwanajamii anapofanya kosa, hasa lile ambalo litaathirishabaha zetu, kwa
mfano, tunashawishika kuwa na hasira wakati huo ni muda muafaka tunaotakiwa
kuwa kimya. |
..
| Tunapoona
mtu amefanya makosa yanayoweza kuharibu matokeo ya kazi yetu, tunapata
hasira na ni jukumu letu kujitahidi kuimudu hiyo hasira. Njia mojawapo
ya haraka ni kwenda matembezi. Kama hakuna muda wa kutosha, basi nenda
katika chumba kingine bila kuonyesha hasira yako, na utulize hasira zako
huko mbali na yule aliyekukosea. |
. |
Na
baada ya kutuliza hasira zako utakuwa tayari kuendelea tena na kazi iliyokuletea
hasira.Kama ilisababishwa na mteja, mfanyakazi au mtu wa kujitolea chukua
hatua zinazoonyeshwa kwenye maneno muhimu. KosaHicho
kitendo kitakuwa na manufaa tu kama tutakifanya wakati tumetulia, na kujiweka
sawa tena. |
.
..
––»«––
|