Tafsiri:
Arabic
English
Español
Filipino
Français
Hindi
Italiano
Japanese
Korean
Malay
Português
Romãnã
Aina
zengine:
Ufahamu
Kurasa nyingine:
Yaliyomo:
Yaliyomo:
|
KUCHANGIA
MAWAZO; TARATIBU
NA MTINDO
imetafsiriwa
na Lillian Naka
Utaratibu
wa mbinu
Mbinu
katika matayarisho ya uwezeshaji wa jamii
Mwongozo
huu utakuwezesha kukisaidia kikundi kufanya uamuzi kwa pamoja.Mbinu hii yaweza kutumika
kwenye mkutano wa kijamii,mkutano wa viongozi wa shirika la kijamii,viongozi wa mashirika
yasiyo ya kiserikali,shirika la kiserikali au shirika la umoja wa mataifa, kati ya
washiriki watano hadi mia mbili.
Maadamu
una ujuzi wa kukiongoza kikao na utahakikisha mtindo na kanuni za kikao zimefuatwa
(kwa mfano, hakuna kukosoa au kumsuta mwengine), utakuwa unahakikisha kuwa maamuzi
ni ya kundi zima na wala hayakulazimishwa na uwepo wako.Utakuwa una sahilisha uamuzi
wa kundi.
Madhumuni
ya kikao cha kuchangia mawazo:
Madhumuni
ya kikao cha kuchangia mawazo ni kutambua shida na kutafuta kwa pamoja, uamuzi mwafaka
wa kutatua shida hiyo.
Mahitaji;
- Shida
inayohitaji kutatuliwa;
- Kikundi
chenye uwezo wa kufanya kazi kwa pamoja.Hii hutumika kwa kundi la watu wapatao watano
hadi kumi (kwa mfano wafunzi,shirika la wafanyikazi,wanaofanya kazi nje ya ofisi
zao), hadi mkutano wamamia ya wanakijiji;
- Ubao,kurasa
za karatasi kubwa au kitu ambacho kitaonekana vyema na wote, na kalamu zenye maandishi
manene;na
- Msahalishi(wewe).Mtu
ambaye jukumu lake ni kuandika vidokezo vya washiriki wala si maoni yake,na utumie
ujuzi wa uongozaji kudhibiti nidhamu na malengo ya kikao.
Kanuni
za kimsingi:
- Msahalishi
ataongoza kila kikao;
- Msahalishi
ataalika washiriki kutoa vidokezo;
- Hakuna
kukosoa (dokezo la mwengine);na
- Vidokezo
vyote viandikwe ubaoni (hata vile visivyostahili)
Taratibu:
- Fasili
au tambua shida:
- Uliza
vidokezo juu ya shida muhimu;
- Hakuna
kukosoa dokezo la mwengine;
- Andika
shida zote zilizodokezwa ,ubaoni
- Ziweke
pamoja, shida zinazoambatana au kuhusiana;kisha
- Ziandike
upya kulingana na umuhimu (zenye umuhimu mkubwa ziwe juu).
- Zalisha
Lengo:
- Pindua
fasili ya shida (suluhisho lake)
- Suluhisho
la shida iliyofasiliwa hapo juu, ndilo lengo
- Fasili
lengo kama suluhisho la shida;
- Andika
lengo hilo ubaoni; kisha
- Likumbushe
kundi kwamba lengo hilo ndilo walilo chagua
- Fasili
Nia au shabaha:
-
- Elezea
tofauti kati ya shabaha au Nia na Lengo;
- Msahalishi
anastahili kufahamu haya:(Tazama HODARI;Shabaha,
yaweza kukadiriwa,ina kiwango na tarehe ya kumalizika).
- Uliza
kundi litoe vidokezo kuhusu shabaha;
- Andika
vidokezo vyote kuhusu shabaha, Ubaoni;
- Hakuna
anayepaswa kukosoa (kidokezo cha mtu yeyote);
- Viweke
pamoja, vidokezo vinavyohusiana au kuambatana;
- Viandike
upya kulingana na umuhimu wake (vyenye umuhimu mkubwa viwe juu);kisha
- Wakumbushe
washiriki wa kundi kuwa, ni wao, waliozalisha shabaha hizo.
- Tambua
rasilimali na vizuizi:
- Uliza
kundi litoe vidokezo kuhusiana na rasilimali na vizuizi;
- Viandike
vidokezo vyote kuhusiana na rasilimali na vizuizi, ubaoni;
- Hakuna
anayepaswa kukosoa (kidokezo cha mshiriki yeyote);
- Ziweke
pamoja rasilimali zinazofanana au kuhusiana.
- Ziandike
upya kulingana na kipaumbele (zenye umuhimu mkubwa ziwe juu).
- Likumbushe
kundi kuwa, ni wao waliozalisha orodha hiyo;
- Viweke
pamoja , vizuizi vyote vinavyofanana au vinavyoambatana.
- Viandike
upya kulingana na kipaumbele(vyenye umuhimu mkubwa viwe juu);kisha
- Likumbushe
kundi kuwa, ni wao waliozalisha orodha hiyo.
- Tambua
mbinu:
- Uliza
kundi litoe vidokezo kuhusu mbinu zitakazotumika;
- Viandike
vidokezo vyote ubaoni;
- Hakuna
apaswaye kukosoa (kidokezo cha mwengine)
- Viandike
pamoja, vidokezo vinavyoambatana au vinavyohusiana ;
- Viandike
upya kulingana na kipaumbele (vyenye umuhimu mkubwa viwe juu);
- Likumbushe
kundi kuwa, ni wao waliozalisha orodha hiyo;
- Chagua
mtindo ulio juu ya orodha.
- Andika
ubaoni, maamuzi ya kundi kwa ufupi:
- shida;
- lengo;
- shabaha
au Nia;
- rasilimali
- vizuizi;
na
- mtindo;
Elezea
kundi kwamba, wametengeza mpangilio wa vitendo vitakavyotumika. Ikiwa mtu ataandka
yaliyoamuliwa katika kila kitengo kilichotajwa hapo juu,atapata kiini cha waraka
wa mpangilio.Waeleze kwamba,wametayarisha mpango huo kwa pamoja na "wanaumiliki".
Mwisho:
Ni
nyepesi.Hii haimaanishi kuwa ni rahisi lakini huboreka ikiwa desturi.kwenye kila
sehemu ya kikao hicho,waweza tumia michezo ya kuigiza,michezo inayojumuisha kundi
na mbinu zengine.Jaribu mitindo tofauti mara kwa mara.
Heri
njema na mafanikio kwenye uchochezi wa jamii!
––»«––
Maamuzi
kwenye mfano huu yametokana na maswali
yale manne ya msingi kuhusu
usimamizi.Majibu ya maswahili hayo, ,kwa pamoja, ndio kiini cha ushauri
wa mradi.Kama
njia mbadala,kikao cha SWOT chawezatumika
kwa kundi kubwa.
Kikao
cha kuchangia mawazo:
© Hakimiliki 1967, 1987, 2007 Phil Bartle Web Design: Lourdes Sada
––»«––Imeratibishwa
mwisho: 2009.04.30
|