Ukurasa wa nyumbani
 Katikaa Utendaji


Tafsiri:

Arabic
Bahasa Indonesia
Chinese
English
Español
Français
Hindi
Italiano
Japanese
Chinese
Nepalese
Hindi
Polski
Português
Romãnã
Thai
Urdu

Aina nyingine:

Ufahamu

Kurasa zengine

Visomo

Ramani ya tovuti

Maneno muhimu

Wasiliana nasi

Nyaraka za matumizi

Tovuti zinazohusiana

SHEREHE

Mwisho na Mwanzo mpya

na Phil Bartle, PhD

imetafsiriwa na Lillian Odembo Naka


Kifafanuzi cha Mafunzo

Sherehe sio likizo bali ni sehemu muhimu katika utenda kazi

Upangaji na Utekelezaji wa sherehe za kijamii ni kazi ngumu na muhimu katika kuileta jamii pamoja.

Pengine hujagundua kuwa; kwa wanafunzi na wafanya kazi wengi, sherehe ni mapumziko kutoka kwa masomo au kazi. Lakini kwako wewe, sherehe ni moja kati ya majukumu yako.

Kama ilivyo dhahiri wakati wa kusherekea (yaani kumalizika kwa mradi),unapaswa kuhimiza shere zengine katika harakati: kuchangisha pesa, kuweka jiwe la msingi, kupeana cheki, Kumalizika kwa awamu muhimu ( Ukuta, paa, upakaji rangi) na sehemu zingine.

Kupiga ngoma, kudensi, mchezo wa kuigiza, maonyesho ya vipawa na aina zengine za tamasha vyafaa kujumuishwa kwenye kila sherehe. Yaalike makundi ya tamasha kutoka kwenye jamii na shule ili kutumbuiza. Hakikisha watu wenye hadhi kuu wamehudhuria na kutoa hotuba za kuisifu jamii (wala si kugeuza sherehe kuwa kongamano la kisiasa) pia yaalike mashirika ya utangazaji na wanahabari.

Kwa nini?

Sherehe hizo huongeza hamasisho kwa jamii na umma na kulipa nguvu jukumu la ustawishaji wa jamii wala si mradi huo pekeyake

Ni pahali pema pa hamasisho, kuboresha uwazi na kuweka mradi wa kijamii kuwa kitendo chenye hadhi kuu.

Unapaswa kupanga mipango yote pamoja na viongozi wala si kuwafanyia kila kitu.

Himiza, sifu na uwape wasia,- kwamba wanaweza, Tazama"Sherehe."

Burudika.

––»«––
Kumalizika kwa mradi;Sherehe na maadhimisho:

Upigaji ngoma kwenye Sherehe

Imeratibishwa mwisho: 2009.02.09

 Ukurasa wa nyumbani

 Katika Utendajji