Ukurasa wa nyumbani
 Katika utendaji


Tafsiri:

Bahasa
English
Español
Filipino
Français
Italian
Português
Hindi
Urdu

Aina zengine:

Ufahamu

Kurasa zengine

Visomo

Ramani ya tovuti

Maneno muhimu

Wasiliana nasi

Nyaraka za matumizi

Tovuti zinazohusiana

UTEKELEZAJI WA MPANGO WA KIJAMII

Kitendo cha uwezeshaji

na Phil Bartle, PhD

imetafsiriwa na Lillian Odembo Naka


Kifafanuzi cha mafunzo

Kufuatilia mpango ni kufanyika kwa mradi

Katika kipindi cha matayarisho,angalau nyaraka mbili zafaa ziwe zimetayarishwa (na viongozi) na kuidhinishwa (na jamii yote). Nyaraka hizi ni: (1)mpangilio wa utekelezaji wa kijamii, na (2) Mpangilio wa mradi (ambayo yaweza kuwa imetumika katika maombi ya ufadhili).

Nyaraka hizi zitasaidia wakati wa ugomvi au utata wa kinachofaa kufanyika, mpaka pale nyaraka hizo zitakapobadilishwa na viongozi na jamii kwa jumla. Ramani ya mradi inafaa iwe sambamba na mpangilio wa utekelezaji kutoka kwa jamii

Jukumu lako si kufanya kazi, bali ni kuwezesha jamii kujifanyia mpango huo.

Hakikisha watu waliochaguliwa kufanya kazi fulani wanaifanya kazi hiyo. Hakikisha ufuatiliaji wa mradi unafanyika. hakikisha kuna mikutano ya mara kwa mara kwa viongozi (ambapo majadiliano ya maendeleo ya mradi yanafanyika) na mikutano ya jamii kwa ujumla. Hakikisha kumbukumbu sahihi zimehifadhiwa, hasa zile za matumizi ya pesa.

Wasaidie viongozi kuweka kumbukumbu ya jinsi wanavyo fanya kazi na mchango wao katika mradi (masaa wanayo tumia katika mikutano, mipango).kumbukumbu zinafaa kuwekwa kuashiria vile masaa hayo yanavyotafsiri kifedha. Hii inamaanisha, mikutano mingi kati yako na viongozi na mikutano michache ya umma na jamii yote.

––»«––

Kitendo cha jamii; Kuchimba mtaro:


Kitendo cha jamii; Kuchimba mtaro

Ukinakili kutoka kwa tovuvti hii, tafadhali, Mnukuu mwandishi
na uihusishe na tovuti hii www.scn.org/cmp/

Imeratibishwa mwisho: 2008.06.25

 Ukurasa wa nyumbani

 Katika utendaji