Ukurasa wa nyumbani
 Katika utendaji


Tafsiri:

Bahasa Indonesia
English
Español
Français
Italiano
Português
Nepalese
Hindi
Urdu

Aina zengine:

Ufahamu

Kurasa zengine:

Visomo

Ramani ya tovuti

Maneno muhimu

Wasiliana nasi

Nyaraka za matumizi

Tovuti zinazohusiana

MAHITAJI YALIYOZALISHWA NA JAMII

Wala si mahitaji yaliyozalishwa na Shirika

na Phil Bartle, PhD

imetafsiriwa na Lillian Odembo Naka


Kifafanuzi cha mafunzo

Mradi uanzapo,viongozi wanafahamu
zaidi ujuzi unaohitajika

mradi unapoendelea, viongozi na jamii watagundua kwamba wanahitaji ujuzi mpya.

Ujuzi huo waweza kuwa uchoraji,useremala, ujenzi na ujuzi mwingine unaoambatana na ujenzi. Ujuzi zaidi waweza kuwa wa kifedha, kupanga mipango, kuweka kumbukumbu, kuchangisha pesa, kuandika ripoti, kusuluhisha ugomvi na kudhibiti miradi.

Mafunzo yaweza kuwa ya papo hapo kwenye mradi ambapo yule anayefahamu ujuzi fulani ana wafunza wasio jua au yale ya kuhudhuria masomo shuleni aidha zile za serikali au za kibinafsi.

Unapaswa kusisitiza mafunzo ya papohapo kwenye mradi kwa kutumia rasilimali zipatikanazo katika jamii hiyo. Wazee katika jamii hiyo, walio na ujuzi wanaweza kuwafundisha vijana.

Ikiwa Ujuzi unahitajika kukodiwa, ni vyema kukodi kutoka kwa jamii yenyewe na ujumuishe mafunzo ya wale wasioufahamu ujuzi huo (wake kwa waume).Hakikisha viongozi wanaweka kumbukumbu ya mafunzo yeyote ya papohapo kwenye mradi.

Kama mafunzo ya papohapo hayawezekani, waweza taja uwezekano wa mafunzo ya shuleni. Lazima kuwe na bajeti, mahali pesa zitatoka ili kulipia masomo hayo.

Kama makadirio hayo ya mafunzo yatafanywa mapema , yanaweza kujumuishwa kwenye maombi ya ufadhili Kutayarisha warsha.

Kulingana na bajeti, watu zaidi waweza kupelekwa kwenye mafunzo hayo ya shuleni.

Jukumu lako ni kuhakikisha kuwa mafunzo hayo yameidhinishwa na jamii yote, na yana umuhimu katika mradi wala sio tu kumnufaisha mtu mmoja.Pia hakikisha wale watakaohudhuria mafunzo hayo wamechaguliwa na jamii yote ili kuzuia tashwishi za upendeleo.

Ikiwa mafunzo yatahitajika wakati mradi unapoendelea, hakikisha wanaohudhuria wameidhinishwa na jamii yote, ufuatiliaji na rekodi kuhusu masomo yao iwekwe na ijumuishwe kwenye ripoti ya maendeleo.

––»«––

Mkutano wa jamii; Kutathmini mahitaji


Mkutano wa jamii;Kutathmini mahitaji

Imeratibishwa mwisho: 2008.06.25

 Ukurasa wa nyumbani

 Katika utendaji