FAHAMU DHANA ZA MSINGI
Taratibu
na kuwaza kufuatana na Maarifa
na Phil
Bartle,
PhD Imetafsiriwa
na Elie Chansa
Kitini
cha Mafunzo
Dhana
na taratibu ambazo mratibu anatakiwa aelewe
Maendeleo ni
nini? Maendeleo
ya jumuiya?
Ushiriki
kwenye jumuiya? Umaskini? Jumuiya?
Uwezeshaji? Uwazi? Ustahimilivu?
Haya
maneno yamejadiliwa kwenye funguo
za maneno.")
Kuwa
mratibu mwenye mafanikio, unahitaji maarifa machache kwenye mdahalo wa umma na kuongoza
makundi kwa ajili ya vitendo. Unahitaji kujua kwa nini utumie maarifa hayo. Unahitaji
kujua taratibu.
Kama
mlengwa wako ni jamii, basi unatakiwa kujua baadhi ya dhana za kisaikolojia kuhusiana
na asili ya jumuiya na asili ya mabadiliko ya kijamii (ikiwemo maendeleo) ya jumuiya.
Hii
inamaanisha kuwa unahitaji uelewa wa jamii shiriki, maliasili na maendeleo, asili
ya watu, uchumi, siasa, na nguvu pamoja na mchakato unaohusiana na taaluma hiyo.
(Tazama "Tamaduni.")
Kwa
sasa hakuna ulazima wa kuwa na shahada ya chuo kikuu, lakini unatakiwa ujifunze taratibu
na maarifa ya masomo hayo.
Ukitaka kukuza (kuwezesha
)
jamii ya kipato cha chini, unatakiwa umuelewe adui, ambaye ni tatizo sugu la utegemezi.
(Tazama: "Utegemezi").
Kama lengo lako ni kuondoa ama kukomesha
umaskini
unahitaji
kujua zaidi ya dalili na matokeo ya umaskini.
Unahitaji
pia kuelewa chanzo cha umaskini, ili kuunga mkono, na kuchangia mabadiliko yatakayopambana
na sababu hizo.
Unatakiwa
ujue kuwa mbinu za kupunguza umaskini zinapunguza makali kwa muda tu, ila hayachangii
kukomesha umaskini.
Umaskini
siyo suala la
hela,
na hela pekee hazitokomesha umaskini (Tazama "Mbinu
za Kupunguza Umaskini").
Kama
ukitazama "Funguo
za maneno,"
Utapata listi nzuri tu kuhusu dhana za msingi kuhusiana na mfanyakazi wa jamii.
Kati
ya zote, hutopata maana ya kamusi; utapata baadhi ya maelezo kuhusiana na makusudi
ya kijitabu hichi: Jinsi ya kuwa mratibu
Modul
ya hivi karibuni Taratibu
za kuiwezesha Jumuiya,
Itakuonyesha kiundani zaidi taratibbu zinazokuwa nyuma ya mbinu na maarifa ambayo
yapatikana kwenye mtandao huu.
Usikariri
hayo maneno. Fikiri kuhusu kila dhana. Andika kuhusu dhana hizo kwenye jarida lako
Jadili
na wenza katika mikutano, midahalo, ama kwenye mafunzo. Kwa muda wako unapokuwa umepumzika,
baada ya kazi na marafiki, ondoa muda kidogo wa kujadili matokeo ya mpira na badala
yake ujadili dhana mojawapo, au zaidi.
Kujaribu
kujifunza "mara moja tu na kuacha" , ni sawa na kujaribu kula "mara
moja tu na kuacha"
Kujifunza,
kama maendeleo ya jamii, hakutakiwi kuisha. Unapoacha kujifunza, umekufa.
––»«––
© Hakimiliki 1967, 1987, 2007 Phil Bartle Ukurasa umesanifiwa na Lourdes Sada
––»«––Imehakikiwa: 2009.11.01
|